Chama cha wafanyakazi wa Serikali Chatangaza KUMSHITAKI Zitto Kabwe kwa kuutaja mshahara wa Rais hadharani
Posted by Bigie habari za kitaifa 3:33 AMHATUA ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kutaja hadharani mshahara wa Rais na Waziri Mkuu, imechukua sura mpya baada ya Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) kulaani hatua hiyo na kuomba Spika Anne Makinda kuchukua hatua kwa vile ni ukiukaji wa sheria.
Chama hicho kimeeleza kusikitishwa na kitendo hicho kufanywa na Mbunge aliyehusika na upitishaji wa sheria hiyo huku wabunge wenyewe wakiwa wakali pale wananchi na wadau mbalimbali wanapohoji mapato yao.
Katibu Mkuu wa Tughe Taifa, Ally Kiwenge alisema Dar es Salaam jana kwamba pamoja na hatua hiyo kukiuka sheria ya kazi na uhusiano kazini inayosema mshahara ni siri ya mwajiri na mwajiriwa, pia kitendo hicho si ajenda ya wafanyakazi hivi sasa.
Alisema ajenda ya wafanyakazi kwa sasa ni kuona wabunge wanapigana kufa kupona katika kuhakikisha kuwa mshahara wa mfanyakazi unaongezeka kukidhi mahitaji ya mwezi mzima na kuwaondolea mzigo wa mikopo inayowaandama.
“Huu si wakati wa wafanyakazi kutaka kujua mishahara ya Rais au Waziri Mkuu, ajenda yetu kwa sasa ni kuona wabunge wanapigana ili kuboresha mishahara ya wafanyakazi ili ukidhi mahitaji muhimu tofauti na sasa,” alisema Kiwenge.
Alisema pamoja na hilo ni mkakati wa wafanyakazi sasa kuona wabunge wanatumia muda wao uliosalia kabla ya Bunge kuvunjwa kuhakikisha mambo makubwa mawili yanaingizwa katika Katiba mpya, moja ikiwa ni nafasi ya mfanyakazi kikatiba ikoje na pia kuona Katiba mpya inasema nini juu ya hatima ya maslahi ya wafanyakazi.
“Tunataka Katiba mpya itamke wazi juu ya mishahara ya wafanyakazi ili iwe ni ile inayokidhi haja,” alisema.
Aeleza kuwa ni jambo la kusikitisha kuona wabunge wanaanza kutaja mishahara ya viongozi wa taifa hadharani kwa kudhani kuwa ndio njia sahihi ya kuwasaidia Watanzania bila kujua kuwa hatua hiyo itasababisha mgawanyiko wa matabaka na kuligawa Taifa, jambo ambalo ni la hatari.
“Sisi mishahara ya viongozi wote tunaifahamu na hata ya wabunge, lakini sheria inasemaje juu ya kutangaza mshahara wa mtu hadharani? Wafanyakazi wanaweza kuitaja lakini kwa vile wameandaliwa hawafanyi hivyo, wanazingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi.
“Naamini kama wafanyakazi wangekuwa ni watu wa kukusanyana na wangekuwa hawana maadili wangeweza kusema mengi ambayo yangeshangaza jamii lakini hawafanyi mambo kwa kukurupuka au kuutafuta umaarufu usio na msingi,” alisema.
Katibu Mkuu huyo wa Tughe alisema kwa kufuata mfano wa wafanyakazi, viongozi wakiwemo wabunge watoe kauli za kujenga nchi na si zenye kuashiria matabaka na ubaguzi, jambo linaloweza kusababisha migogoro mikubwa na kuliingiza taifa katika machafuko yasiyo na tija,” alisema.
Alisema wabunge wafahamu pia kwamba suala la mishahara litaendelea kubakia kuwa ni la mwajiri na mwajiriwa na ndio maana katika fomu au nyaraka nyingine zinazoelezea majukumu ya wabunge suala la mishahara na marupurupu yao haliwekwi wazi kwa vile ni siri kati yao na taasisi ya Bunge kisheria.
-Habari leo
Mayasa awashangaa wanaodai kuwa ameolewa.....Asema yeye yupo Single na hahitaji ndoa kwa sasa maana bado ni mdogo sana
Posted by Bigie habari za kitaifa 3:26 AMMsanii wa kike wa filamu Bongo, Mayasa Mrisho ( Maya ) amefunguka kuwa wale waliozusha kuwa amechumbiwa ni wanafiki na watasubiri sana mpaka wazeeke kwani suala la ndoa kwake bado halipo leo wala kesho.
Akiongea na mpekuzi wetu, mrembo huyo amedai kwamba uvumi ulionenezwa kuwa amechumbiwa ulikuwa una lengo la kumchafua na kumjaza mikosi ya kupendwa na wanaume.
"Nawashangaa wanaohangaika kuumiza midomo yao wakiwatangazia watu eti nimechumbiwa. Mimi nipo single na sihitaji kuolewa kwa sasa.
"Nahitaji mpenzi wa kufarijiana tu maana ndoa ni kifungo ambacho nadhani sipo tayari kukitumikia katika umri mdogo kama huu"
Mlimani City YASITISHA ukaguzi wa Magari na watu kwa madai kwamba unapunguza wateja
Posted by Bigie habari za kitaifa 2:28 AMSiku chache baada ya kuanzisha ukaguzi wa magari na watu wanaoingia katika maduka ya Mlimani City, ukaguzi huo sasa umesitishwa.
Hatua hiyo ilifuatia tishio la ugaidi baada ya duka la Westgate la Nairobi nchini Kenya kushambuliwa na kikundi cha Al-shabab na kusababisha mauaji ya watu 68 na wengi kujeruhiwa.
Mbali na Mlimani City lililopo Barabara ya Sam Nujoma, jijini Dar es Salaam, maduka mengine makubwa kama vile Quality Plaza lililopo Barabara ya Nyerere nalo lilianzisha ukaguzi kwa wateja wake.
Hata hivyo uchunguzi wa hivi karibuni umebainisha kuondolewa kwa ukaguzi uliokuwa ukifanywa kwa wateja na magari yanayoingia dukani hapo, kwa madai kuwa unapunguza wateja.
Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, askari wa kike wa kampuni ya Omega Nitro inayolinda duka hilo, alisema kuwa hatua hiyo ilikuja Oktoba 16 mwaka huu.
“Nakumbuka Jumatano baada ya kumaliza ‘shift’ niliacha ukaguzi ukiendelea, lakini niliporudi Ijumaa nikaambiwa umesitishwa mara moja,” alisema na kuongeza:
“Kwa kweli ukaguzi wenyewe ulikuwa mgumu kwani hatukuwa na vifaa vya kutosha na wateja ni wengi,” alisema na kuongeza: “Katika ukaguzi tulikuta watu wengi na silaha hasa bastola wakimiliki kihalali.”
Jitihada za kuupata uongozi wa Mlimani City hazikufanikiwa kwa kile kilichoelezwa kuwa yuko likizo. Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura alisema hana taarifa ya kusitishwa kwa ukaguzi, lakini akasisitiza kuwa hilo ni suala lao binafsi.
Rais Kikwete awahimiza wanaume kujitokeza Kutahiriwa ( tohara ) ili kukabiliana na maambukizi ya UKIMWI
Posted by Bigie habari za kitaifa 2:04 AMRAIS Jakaya Kikwete amewataka wanaume kuendelea kujitokeza kwa wingi kupata tohara, kama moja ya njia za kukabiliana na Ukimwi unaoendelea kuua watu wengi.
Akisalimia wananchi katika Kijiji cha Kipengele kilichoko Wilaya ya Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe, ambako anaendelea na ziara yake kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo, aliwapongeza wanaume ambao hadi sasa wamejitokeza kupata tohara kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo.
Aliwaambia wananchi waliohudhuria mkutano wake wa hadhara kuwa kwa mujibu wa wataalamu, majaribio ya tohara ambayo yamekuwa yanaendelea katika Mikoa ya Mbeya, Iringa na Njombe, yameonyesha mafanikio hata kama mikoa hiyo ndiyo inaendelea kuongoza nchini kwa maambukizi ya ugonjwa huo.
“Miaka michache iliyopita, tulianzisha kampeni ya tohara kwa wanaume wa Mikoa ya Mbeya, Iringa na Njombe kwa majaribio na kwa ushauri wa madaktari. Sasa wataalamu wanatuambia kuwa kampeni hiyo imekuwa ya mafanikio makubwa sana.
“Naambiwa kuwa mwitikio wa kampeni hii umekuwa mzuri sana. Endeleeni. Nawapongeza wale ambao wameshiriki shughuli hiyo hadi sasa na kuwashauri wale ambao bado nao wafikirie namna ya kujiunga kwenye kampeni hiyo. Kama wewe bado basi jitahidi ujiunge,” alisema Rais Kikwete.
Hata hivyo, alifafanua kuwa watu wasije kufirikia kuwa tohara pekee yake inatosha kuzuia maambukizi ya Ukimwi.
“Kufanya tohara hakuna maana kuwa mtu hawezi kupata Ukimwi. Tohara sio kinga wala tiba ya Ukimwi kwa sababu tiba na kinga za Ukimwi bado kupatikana.
“Wanachosema wataalamu, hata hivyo, ni kwamba mtu mwenye tohara anayo nafasi kubwa zaidi ya kuepukana kupata Ukimwi kuliko yule ambaye hana tohara na siyo kwa Ukimwi tu bali kwa magonjwa mengi ambayo yanaambukizwa kwa njia ya kufanya mapenzi,” alisema Rais Kikwete.
Rais Kikwete yuko katika ziara ya siku saba katika Mkoa wa Njombe na jana ameingia katika siku yake ya tatu kwa kutembelea Wilaya za Wanging’ombe na Makete.
-Mtanzania
Hii ni Video ya ripoti ya Mauaji ya Westgate iliyoua watu 69 ikiletwa kwako na Mpekuzi Mohammed All wa Jicho Pevu-KTN..Walichokifanya wanajeshi wa Kenya ni AIBU tupu
Posted by Bigie habari za kitaifa 10:07 AMZimekuwa ni siku nyingi za kubashiri kuhusu kilichojiri wakati wakenya walipotekwa nyara na magaidi kwa siku nne mtawalia.
Wakenya zaidi ya sitini walipoteza maisha yao katika jumba la Westgate lakini hadi sasa Wakenya hawajajua ukweli kuhusu yaliyojiri katika jumba la Westgate.
- Je ni kweli kuna waliokuwa wametekwa nyara na magaidi na kuzuiliwa katika jumba hilo?
- Je ni kweli kuna magaidi waliouawa na wanajeshi?
Meza ya upekuzi ya Jicho Pevu na Inside Story usiku na mchana wamekuwa wakidurusu kila ukurasa na kufanya mahojiano na kupitia hatua kwa hatua video za CCTV kutoka jumba la Westgate na sasa wako tayari kukusimulia kilichojiri.
Ungana na mwanahabari mpekuzi Mohammed Ali kwenye video ya KTN iliyopachikwa hapo chini...
Mpira umekwisha: Yanga 3, Simba 3
Posted by Bigie habari za kitaifa 8:07 AMPambalo la yanga na Simba limekwisha kwa sare ya 3:3
Majumuisho:
Dk 90+5 FULL TIME! Simba 3-3 Yanga
Dk 83 .. Gilbert Kaze anaipatia Simba bao la tatu akiunganisha krosi safi ya faulo iliyopigwa na Chollo. Simba 3-3 Yanga.
Dk 72 Mpira umebadilika na Simba sasa wametawala mchezo.
Dk 67 Mpira umesimama kwa muda baada ya Tambwe kuumia.
Dk 64 Ngassa anakosa bao la wazi akiwa amebaki na kipa.
Dk 61 SUB: Yanga imefanya mabadiliko ametoka Kiiza ameingia Simon Msuva.
Dk 60 YELLOW CARD...! Singano anaonyeshwa kadi ya njano.
Dk 59 Simba wamebadilika na wanacheza soka safi sasa.
Dk 57 GOOOOO.....! Joseph Owino anaipatia Simba bao la pili kwa kichwa akiunganisha mpira wa kichwa. Simba 2-3 Yanga.
Dk 56 Simba inapata kona.
Dk 54 GOOOOO....! Mombeki anaipatia Simba bao la kwanza akimalizia pasi nzuri ya Tambwe. Simba 1-3 Yanga.
Dk 53 Niyonzima anakosa bao la wazi.
Dk 48 SUB: Simba imefanya mabadiliko wametoka Abdulhalim Humud na Chanongo wameingia William Lucian na Said Hamisi. Simba 0-3 Yanga
Dk 45 KIPINDI CHA PILI KIMEANZA!
Half time - Yanga 3 - 0 Simba
Dk 45 ! Kiiza anaipatia Yanga bao la tatu akiunganisha vyema pasi ya Kavumbagu. Simba 0-3 Yanga. Simba 0-3 Yanga.
Dk 43 Cannavaro anamchezea rafu Amisi Tambwe.
Dk 41 Licha ya Yanga kuongoza kwa mabao 2-1, mashabiki watatu wa Yanga wamezimia na kupewa huduma ya kwanza.
Dk 41 Chanongo anamchezea rafu Mbuyu Twite wa Yanga.
Dk 38 Yanga wanapiga pasi 18 bila Simba kugusa.
Dk 35 .! Kiiza anaipatia Yanga bao la pili akiunganisha mpira uliodokolewa na Kavumbagu aliyeugusa mpira uliorushwa na Mbuyu Twite. Simba 0-2 Yanga.
Dk 32 YELLOW CARD...! Mkude wa Simba anaonyeshwa kadi ya njano.
Dk 26 David Luhende anakosa bao la wazi baada ya shuti lake kutoka nje kidogo ya lango la Simba.
Dk 25 Kiiza anamchezea rafu Chanongo.
Dk 24 Yanga inapata kona lakini Simba wanaokoa.
Dk 23 Kavumbagu anakosa bao la wazi baada ya kipa Dhaira kuwahi kuudaka mpira.
Dk 18 Kavumbagu anamchezea rafu Ramadhan Chanongo.
Dk 15 YELLOW CARD...! Ngassa anaonyeshwa kadi ya njano kwa kuchelewesha muda.
Dk 14 ..! Mrisho Ngassa anaipatia Yanga bao la kwanza akiunganisha vyema krosi ya Kavumbagu. Simba 0-1 Yanga
Dk 13 Timu zinashambuliana kwa zamu lakini kazi ipo kwa Cannavaro na Mombeki.
Dk 9 YELLOW CARD...! Mombeki anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea rafu Cannavaro. Rafu hii ni ile ya kwanza.
Dk 7 Betram Mombeki wa Simba anapiga kichwa langoni kwa Yanga lakini kipa Ali Mustapha anaudaka mpira.
Dk 7 Niyonzima anamchezea rafu Abdulhalim Humud wa Simba.
Dk 4 Ngassa anapiga krosi safi langoni kwa Simba lakini Kiiza anachelewa kuunganisha.
Dk 3 Jonas Mkude anamchezea rafu Mrisho Ngassa wa Yanga.
Dk 2 Yanga wamecheza pasi 10 bila Simba kugusa.
Dk 00 MPIRA UMEANZA!
Mpira umezidi Kukolea: dakika ya 83 simba wanajipatia bao la 3
Posted by Bigie habari za kitaifa 7:53 AMNi kipindi cha pili Simba 2, Yanga 3
Posted by Bigie habari za kitaifa 7:46 AMUPDATE:Julius Nyaisanga (Mtangazaji wa zamani Radio One na Mkurugenzi wa Abood Media) afariki dunia
Posted by Bigie habari za kitaifa 3:45 AMAliyekua mkurugenzi wa Abood media bwana Julius nyaisanga,amefariki dunia huko Morogoro katika hospitali ya Mazimbu...
Marehemu aliwahi pia kufanya kazi katika kituo cha Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na katika Kituo cha Redio One ambapo alikuwa Mkurugenzi.
Mpaka sasa chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika japo marehemu alikuwa akiugua kwa muda mrefu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN!
Wema Sepetu afunguka na kudai kwamba yeye hampendi DIAMOND bali anapenda PESA zake.
Posted by Bigie habari za kitaifa 1:10 AMBaada ya wadau na mashabiki wake kuubariki uhusiano wake na Diamond huku wakimponda Penny na kudai amezeeka na kwamba hamfai Diamond, mrembo huyo ameamua kuwajibu mashabiki hao kwa lugha ya fumbo la picha.
Jana mrembo huyo alitupia picha mtandaoni kuonyesha msimamo wa fikra zake juu ya penzi la Diamond.
Kwa mujibu wa picha hiyo,anachokitaka Wema Sepetu toka kwa Diamond ni PESA na siyo ndoa au mapenzi ya dhati kama mashabiki wake wanavyodhani.
===Mke mwema hutoka kwa Mungu na mume mwema hutoka Benki====
Lulu Michael afunga na kuomba kwa ajili ya hukumu ya Babu Seya ambayo itasikilizwa tena tarehe 30 mwezi huu
Posted by Bigie habari za kitaifa 12:02 AM
Haya ni maneno ya mwanadada Elizabeth Michael (LULU) aliyoyaandika mtandaoni akiwaombea kheri Mzee Nguza na mwanawe Papii Kocha wanaosubiria kusikilizwa upya kwa kesi yao iliyowafanya wafungwe kifungo cha maisha jela.
“Ninaamini Mungu yupo...anasikia,anaona na ndiye mwenye kuhukumu kwa Haki...!!!! Dua zangu ziko pamoja na Mzee Nguza na Papii Kocha...!
"Hakuna linaloshindikana mbele ya Mwenyezi Mungu...Kama anaweza kutoa Jaribu basi yeye pia ndo mwenye Uwezo wa kufanya Njia ya kutoka ktk jaribu Hilo...Mwenyezi Mungu awasimamie katika rufaa yenu...! AMEN”
“Ninaamini Mungu yupo...anasikia,anaona na ndiye mwenye kuhukumu kwa Haki...!!!! Dua zangu ziko pamoja na Mzee Nguza na Papii Kocha...!
"Hakuna linaloshindikana mbele ya Mwenyezi Mungu...Kama anaweza kutoa Jaribu basi yeye pia ndo mwenye Uwezo wa kufanya Njia ya kutoka ktk jaribu Hilo...Mwenyezi Mungu awasimamie katika rufaa yenu...! AMEN”
CCM wamsaliti Kikwete....Wadai kwamba wako tayari bunge livunjwe na uchaguzi ufanyike kabla ya 2015 lakini siyo kufanya marekebisho ya WAPINZANI
Posted by Bigie habari za kitaifa 10:30 PMHOFU kubwa imetanda ndani na nje ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), juu ya upatikanaji wa katiba mpya, hasa baada ya Rais Jakaya Kikwete kusaini muswada ambao sasa ni Sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba.
Mkutano kati ya Rais Kikwete na viongozi wa vyama vya siasa vyenye uwakilishi bungeni uliofanyika Ikulu Oktoba 15, 2013 umeongeza mpasuko ulioanza kujitokeza baina ya makada wa CCM na wapinzani.
Katika mkutano huo, rais na viongozi wa upinzani waliafikiana vyama vyote vya siasa nchini vyenye mawazo, maoni na mapendekezo ya kuboresha Sheria ya Kurekebisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba viwasilishe mapendekezo yao haraka serikalini ili ifatutwe namna ya kuyashirikisha katika marekebisho ya sheria hiyo.
Walikubaliana kwamba vyama vya siasa nchini, kama wadau muhimu katika mchakato wa katiba mpya, viangalie namna ya kukutana na kujenga mfumo wa mawasiliano na maridhiano wa jinsi kwa pamoja vitakavyosukuma mbele mchakato huo kwa masilahi mapana ya nchi yao na mustakabali wa taifa.
Awali kabla ya mkutano huo, makada wa CCM wakiwamo mawaziri kadhaa waliweka wazi kuwa milango ya Ikulu imeshafungwa kwa wapinzani kuzungumzia suala hilo, lakini Rais Kikwete alipotangaza kukutana nao iliwaweka njia panda.
Tanzania Daima limedokezwa kuwa baadhi ya makada wa CCM wamekuwa wakimshutumu Rais Kikwete kwa kuwabembeleza wapinzani huku akikiumiza chama chake.
Hoja wanayoijenga ni kuwa Rais Kikwete anataka kujijengea kitu cha kukumbukwa, hasa katika suala la katiba mpya bila kujali athari zinazokipata chama chake.
Makada hao wanaweka bayana kuwa hali hiyo itakiacha chama katika wakati mgumu wa kukabiliana na wapinzani wanaoonekana kuimarika kadiri siku zinavyoyoyoma.
Baadhi ya wabunge wa CCM wanamuona Kikwete kama msaliti kwa wabunge wake waliopitisha muswada huo, ambao sasa ni Sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba, ukiwa na upungufu ulioainishwa na wapinzani.
Mmoja wa watu waliohudhuria mazungumzo ya Ikulu anasema rais aliridhia marekebisho hayo na alibainisha kuwa yajikite katika masuala kadhaa, likiwamo suala la Tume ya Warioba kuwapo kwenye Bunge Maalumu la Katiba, marekebisho katika suala la uteuzi wa wajumbe 166 ili idadi iongezeke na hoja ya Zanzibar kushirikishwa kabla ya muswada wa sheria ya kura za maoni kuanza.
Tayari Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba, alishatoa tamko kuwashangaa wabunge wa CCM kwa kupotosha kifungu kilichokuwa kinasema Tume ya Mabadiliko ya Katiba itavunjwa na rais mara tu baada ya kuwasilisha rasimu kwenye Bunge Maalumu la Katiba, msimamo ambao unaungwa mkono na Mbunge wa Nzega, Hamis Kigwangala (CCM).
Mbunge huyo katika andiko lake alilolisambaza katika vyombo vya habari, anakiri kuwa moja ya upungufu alioubaini katika muswada ule ambao sasa ni sheria, ni kuiua Tume ya Mabadiliko ya Katiba kabla ya mchakato kufikia mwisho.
“Kiukweli, lina mantiki ndani yake. Tukiwa kwenye Bunge la Katiba hakutakuwa na serikali, sasa ni nani atakayejibu na kuweka sawa hoja za wabunge? Hili kwa kweli wabunge tuliopitisha muswada ule hatukuliona vizuri,” alisema Kigwangala.
Wakati Kigwangala akiona upungufu huo, Naibu Spika Job Ndugai, anajitetea kuwa haoni udharura wa suala hilo kurejeshwa bungeni.
Ndugai amebeza suala la urejeshwaji wa sheria hiyo bungeni, akihoji kuwa suala hilo halina udharura.
“Ni ishu gani hasa ambayo wapinzani walienda kumwona rais ambayo inahitaji udharura huo? Je, kanuni za Bunge zinaruhusu suala hilo?” alihoji Ndugai.
Akizungumza na mwandishi wetu wiki hii, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema Bunge ni muhimili tofauti.
Wabunge kama wataona kuna kitu cha kubadilisha watabadilisha, lakini wakiona hakuna cha kubadilisha itabaki ilivyo.
Kauli hiyo imeungwa mkono jana na Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe, ambaye alinukuliwa na gazeti moja nchini , akisema: “Serikali haikusudii kufanya marekebisho yoyote kwenye Sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba iliyosainiwa na Rais Kikwete hivi karibuni.”
Mmoja wa wabunge wa CCM aliyehojiwa na mwandishi wetu na kutoa msimamo wake baada ya rais kusaini muswada kuwa sheria ni aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM, Hamad Yusuf Massauni, ambaye sasa ni Mbunge wa Kikwajuni.
“Mimi ningekuwa rais nisingepoteza muda kuongea na wapinzani, na hata kama sheria hii itarejeshwa bungeni, sioni sehemu yoyote ya kufanyia marekebisho, iwe ya kuondoa koma wala kuweka nukta,” alisema.
Kabla ya muswada huo kusainiwa kuwa sheria, Nape alinukuliwa akisema: “Hofu yangu ni kuwa rais asiposaini muswada huo, ataingia katika mgogoro kikatiba, itabidi arejeshe muswada bungeni aeleze kwanini hajasaini, na ukirejeshwa bungeni wabunge wa CCM wakakataa kufanya mabadiliko, rais angelazimika kuvunja Bunge.”
Aliongeza kuwa: “Mimi ninaona afadhali rais asaini muswada huu ili kama kuna upungufu uwekwe mezani kama ilivyokuwa mwanzo, ila nakubali kabisa mzee Warioba ana hoja katika suala la kutovunjwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kabla ya kutetea rasimu mbele ya Bunge Maalumu la Katiba.”
Alisema wabunge wa CCM ni asilimia 74 ya wabunge wote, hivyo wakishikilia hoja ya kutobadilisha jambo lolote katika muswada huo baada ya kurejeshewa na rais, matokeo yake ni kuvunjwa kwa Bunge na nchi kuingia kwenye uchaguzi kabla ya 2015.
Nape alisema CCM haiko tayari kuingia kwenye uchaguzi kabla ya 2015, hivyo akawataka wanaopinga na kuunga mkono hoja hizo watumie busara na hekima kufikia maridhiano yatakayolijenga taifa.
Alisema kuwa muswada wa mabadiliko ya sheria wa mwanzo nao ulipitishwa ukiwa na kasoro mwaka 2011, lakini Chama cha Demokrasia na Maendeleo walienda kwa rais wakajadiliana wakakubaliwa, na kwamba viongozi wa CCM walilazimika kwenda Dodoma kuwaeleza wabunge msimamo wa Rais Kikwete na kuwashawishi waukubali.
“Tulipoona kuna hoja tulilazimika kwenda Dodoma kuwaomba wabunge wetu wakubali hoja za CHADEMA ili marekebisho yafanyike, ingawa suala hilo lilifanyika kwa taabu sana, sasa zamu hii wabunge wa CCM wanaweza wasikubali hoja za wapinzani, na likiendelea vile rais atalazimika kuvunja Bunge, hili suala limetuweka pabaya sana CCM, sijui hatima yetu,” alisema.
Tanzania Daima , limedokezwa kuwa iwapo serikali itaridhia marekebisho yaliyotajwa na wapinzani, mvutano mkubwa utazuka bungeni kati ya washindi na washindwa.
Jambo hilo linadaiwa halitakubaliwa na wabunge wa CCM ambao mara kwa mara wamekuwa wakishutumiwa kupitisha mambo kwa kuangalia zaidi masilahi ya chama kuliko taifa.
Kumekuwa na mipango ya CCM kumuandaa Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, kuwa Spika wa Bunge la Katiba.
Inadaiwa Chenge ndiye atakayebeba jukumu la kudhibiti baadhi ya hoja zinazopingwa na CCM zilizotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya uenyekiti wa Jaji Joseph Warioba.
Miongoni mwa mambo yaliyomo ndani ya rasimu ya katiba ni serikali tatu.
-Tanzania daima
Leo ni kiama uwanja wa taifa jijini Dar...Nani ATAMPAKATA mwenzake?...Yanga au Simba???
Posted by Bigie habari za kitaifa 9:58 PMWatani wa jadi nchini Simba na Yanga leo jioni wanashuka katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kupambana katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, huku Simba ikiwa na rekodi nzuri ya kuifunga Yanga mabao 5.
Kila upande umekuwa ukitamba kuibuka na ushindi hii leo.
=====YETU MACHO=======
Mama mwenye UKIMWI amchukua mtoto wa jirani na kumnyonyesha maziwa yake....Serikali yamkamata na kumfunga miaka miwili jela
Posted by Bigie habari za kitaifa 1:08 PMMWANAMKE mmoja raia wa Zimbabwe aliyenyonyesha mtoto wa jirani bila ruhusa anakabiliwa na kifungo cha karibu miaka miwili kwa kumwambukiza mtu HIV kwa kukusudia kwa kuwa yeye ni mwathirika.
Mpariwa alikamatwa wiki jana kwa mashtaka ya usumbufu na iwapo mtoto huyo atapatikana na virusi, mashtaka hayo yatazidishwa hadi 'kumwambukiza mtu mwingine HIV kimakusudi.’
Mama wa mtoto huyo wa miezi 14, Nyasha Mironga, alisema kumwona mwanawe akinyonyeshwa na jirani wake lilikuwa ni jambo lililomshtua sana.
Kisa hicho kimetokea baada ya kupitishwa kwa sheria mpya ya HIV/Aids inayotoa adhabu kali zaidi kwa wale wanaowaambukiza wengine HIV kimakusudi
Rais Kikwete asimikwa uchifu wa kabila la Wabena mkoani Njombe
Posted by Bigie habari za kitaifa 7:13 AMRais Jakaya Kikwete akipokea Mkuki wakati akisimikwa Uchifu wa Kabila la Wabena na mmoja wa wawakilishi wa Wazee wa Kabila hilo,kwenye wa Hafla ya Uzinduzi wa Mkoa wa Mpya wa Njombe.
Wazee wa Kabila la Wabena wakimsimika Uchifu Rais Jakaya Kikwete.
Chifu Mpya wa Kabila la Wabena,Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia wakazi wa Mkoa Mpya wa Njombe.
Chifu Mpya wa Kabila la Wabena,Rais Jakaya Kikwete akiteremka Jukwaani baada ya kusimikwa Uchifu wa Kabila hilo na kuwahutubia wananchi wa Mkoa wa Njombe.
Rais Jakaya Kikwete akipongezwa na Mkewe Mama Salma Kikwete baada ya kusimikwa Uchifu wa Kabila la Wabena,wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Mkoa wa Mpya wa Njombe.
Rais Kikwete azindua kiwanda cha Chai mkoani Njombe
Posted by Bigie habari za kitaifa 7:06 AMRais Jakaya Kikwete akifunua kitambaa kwenye jiwe la msingi wakati akizindua kiwanda kipya cha chai cha Ikanga, Njombe, ikiwa ni sehemu ya sherehe za uzinduzi rasmi wa mkoa mpya wa Njombe Ijumaa Oktoba 18, 2013.Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mufindi Tea Company Group Bwana Noel Smith
Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mufindi Tea Company Group Bwana Noel Smith kabla ya kuzindua kiwanda kipya cha chai cha Ikanga, Njombe, ikiwa ni sehemu ya sherehe za uzinduzi rasmi wa mkoa mpya wa Njombe Ijumaa Oktoba 18, 2013.
Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakikagua chai ikichambuliwa katika kiwanda cha chai cha Ikanga, Njombe, ikiwa ni sehemu ya sherehe za uzinduzi rasmi wa mkoa mpya wa Njombe Ijumaa Oktoba 18, 2013.
Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipata maelezo ya kiwanda kipya cha chai cha Ikanga, Njombe,kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mufindi Tea Company Group Bwana Noel Smith baada ya kukizindua ikiwa ni sehemu ya sherehe za uzinduzi rasmi wa mkoa mpya wa Njombe Ijumaa Oktoba 18, 2013.
Taarifa ya lile jambazi la kike lililopigwa kichwa na mteja wakati likijaribu kupora duka la M-pesa kwa bastola
Posted by Bigie habari za kitaifa 6:39 AMJaribio la kupora fedha katika kituo cha M-Pesa lililofanywa na Anita Kaburu (27), pamoja na mwenzake wakitumia bastola na bunduki, lilishindikana baada ya mteja mmoja kumpiga kichwa na kufanikiwa kumdhibiti.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema jana kuwa Anita ambaye ni mkazi wa Usa River wilayani Arumeru, alivamia kituo cha M-Pesa kinachomilikiwa na Stela Mrema akiwa na mwanamume mmoja.
Alisema watu hao wanaodaiwa kuwa ni majambazi, baada ya kufika kwenye kituo cha huduma hiyo maeneo ya Shamsi jijini hapa majira ya saa 6:00 mchana wakijifanya wateja, ghafla mmoja wao (Anita) alichomoa bastola kwenye mkoba wake na mwenzake akatoa bunduki na kuamrisha wapewe fedha.
“Baada ya kuingia walijifanya kuhitaji huduma ya M-Pesa, ghafla yule mwanamke alitoa bastola kwenye mkoba wake na mwanaume naye alitoa bunduki na kuwaamuru watoe pesa na simu… ndipo yule mteja alimpiga kichwa yule mwanamke na kisha kupiga kelele za kuomba msaada hivyo walifanikiwa kumdhibiti,” alisema.
Hata hivyo, alisema mwenzake alifanikiwa kukimbia. Alisema baada ya polisi kumtaka Anita awataje wenzake, polisi waliwakamata watuhumiwa wanne waliokuwa wamepanga kufanya uporaji huo.
Kamanda Sabas aliwataja waliokamatwa kuwa ni Abdulahman Jumanne Idd (27) ambaye ni mwangalizi wa Kampuni ya Ulinzi ya KK na mkazi wa Shamsi, Simon Martine au Mapanki (45) mkazi wa Kwa Mrombo, Hashimu Ally (30) ambaye ni mpanda milima na mkazi wa Ngarenaro na Charles Luangano (24) ambaye pia ni mlinzi wa kampuni ya ulinzi ya KK.
Alisema watuhumiwa hao baada ya kufanyiwa upekuzi walikamatwa na bunduki aina ya shotgun, bastola aina ya bereta na risasi sita za bastola. Alisema watafikishwa mahakamani Jumatatu.
-Nipashe
Kanisa lagoma kumzika yule mwanaume aliyempiga risasi Mtangazaji wa ITV (Ufoo Saro )....Ladai kifo chake kina UTATA.
Posted by Bigie habari za kitaifa 6:38 AM
Familia ya Anthery Mushi, aliyejiua kwa kujipiga risasi Jumapili iliyopita baada ya kumuua kwa risasi mkwewe, Anastazia Saro, amezikwa bila huduma ya kikanisa kijijini kwao Ongoma.
Kanisa Katoliki, Parokia ya Uru ilishindwa kutoa huduma hiyo kutokana na mazingira ya kifo chake.
Licha ya hali hiyo kujitokeza, familia hiyo, ilionyesha nia yake ya kwenda kumuangukia Paroko wa Parokia wa Kanisa hilo, ili aridhie familia ya Anthery, isome misa maalumu ya kuomba ndugu yao afutiwe dhambi inayomkabili.
Mushi (40), alijipiga risasi baada ya kumuua mkwewe na kumjeruhi mzazi mwenziwe Ufoo Saro, mtanzangazi wa kituo cha televisheni cha ITV, eneo la Kibamba CCM, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Wakati familia ya Mushi ikiazimia hilo, kiongozi aliyeteuliwa na familia kufanya ibada ya maziko, baba mdogo wa Mushi, Ugolin Mushi alisema kuwa Watanzania wanapaswa kutomhukumu kwa alichokitenda na kwamba imetosha kwa kuwa kinachoelezwa kila kona ya nchi baada ya tukio hilo ni sawa na mbu kubadilika na kuwa tembo.
“Sisi ni nani hadi tumhoji Mwenyezi Mungu juu ya kilichotokea maana mbu anaweza kubadilika na kuwa mkubwa kama tembo kutokana na habari zinazotangazwa.
"Anayejua ukweli huu ni Anthery na Mungu wake…Lakini Mungu amsamehe makosa yake wakati wa vita na wakati wa amani, wakati wa kuhifadhi na wakati wa kutupa na akafurahi na malaika huko aendako,” alisema.
Hata hivyo, mtoto wa marehemu, Alvin Anthery, ambaye amezaa na Ufoo, hakuweza kumzika baba yake kutokana na sababu zisizojulikana.
Hali ilikuwa tulivu nyumbani kwa marehemu Kijiji cha Ongoma, Uru Kaskazini, tofauti na matarajio ya wengi baada ya kuwasili kwa mwili huo usiku wa kuamkia jana, ingawa mamia ya wakazi wa Uru walifurika kushuhudia mazishi ya Anthery ambaye amelitikisa taifa kwa siku kadhaa kutokana na tukio la mauaji Oktoba 13, kugonga vichwa vya habari.
Juzi, familia ya Anthery, ilinukuliwa wakati wa kuuaga mwili wake katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN), ikiliomba Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina kutokana na ndugu yao kukutwa na risasi mbili.
Mwili wake baada ya kufanyiwa uchunguzi na madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ulikutwa na risasi mbili, moja ikiwa kwenye ubongo na nyingine kwenye jeraha lililo pembeni ya sikio.
Licha ya kanisa kutotoa huduma ya ibada ya mazishi ya Anthery, watawa wa kanisa waliohudhuria katika msiba huo walishindwa kuendesha ibada kutokana na taratibu za kanisa.
Kanisa Katoliki, Parokia ya Uru ilishindwa kutoa huduma hiyo kutokana na mazingira ya kifo chake.
Licha ya hali hiyo kujitokeza, familia hiyo, ilionyesha nia yake ya kwenda kumuangukia Paroko wa Parokia wa Kanisa hilo, ili aridhie familia ya Anthery, isome misa maalumu ya kuomba ndugu yao afutiwe dhambi inayomkabili.
Mushi (40), alijipiga risasi baada ya kumuua mkwewe na kumjeruhi mzazi mwenziwe Ufoo Saro, mtanzangazi wa kituo cha televisheni cha ITV, eneo la Kibamba CCM, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Wakati familia ya Mushi ikiazimia hilo, kiongozi aliyeteuliwa na familia kufanya ibada ya maziko, baba mdogo wa Mushi, Ugolin Mushi alisema kuwa Watanzania wanapaswa kutomhukumu kwa alichokitenda na kwamba imetosha kwa kuwa kinachoelezwa kila kona ya nchi baada ya tukio hilo ni sawa na mbu kubadilika na kuwa tembo.
“Sisi ni nani hadi tumhoji Mwenyezi Mungu juu ya kilichotokea maana mbu anaweza kubadilika na kuwa mkubwa kama tembo kutokana na habari zinazotangazwa.
"Anayejua ukweli huu ni Anthery na Mungu wake…Lakini Mungu amsamehe makosa yake wakati wa vita na wakati wa amani, wakati wa kuhifadhi na wakati wa kutupa na akafurahi na malaika huko aendako,” alisema.
Hata hivyo, mtoto wa marehemu, Alvin Anthery, ambaye amezaa na Ufoo, hakuweza kumzika baba yake kutokana na sababu zisizojulikana.
Hali ilikuwa tulivu nyumbani kwa marehemu Kijiji cha Ongoma, Uru Kaskazini, tofauti na matarajio ya wengi baada ya kuwasili kwa mwili huo usiku wa kuamkia jana, ingawa mamia ya wakazi wa Uru walifurika kushuhudia mazishi ya Anthery ambaye amelitikisa taifa kwa siku kadhaa kutokana na tukio la mauaji Oktoba 13, kugonga vichwa vya habari.
Juzi, familia ya Anthery, ilinukuliwa wakati wa kuuaga mwili wake katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN), ikiliomba Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina kutokana na ndugu yao kukutwa na risasi mbili.
Mwili wake baada ya kufanyiwa uchunguzi na madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ulikutwa na risasi mbili, moja ikiwa kwenye ubongo na nyingine kwenye jeraha lililo pembeni ya sikio.
Licha ya kanisa kutotoa huduma ya ibada ya mazishi ya Anthery, watawa wa kanisa waliohudhuria katika msiba huo walishindwa kuendesha ibada kutokana na taratibu za kanisa.
CHANZO: NIPASHE
Zitto Kabwe adai kwamba yupo tayari CHADEMA na CCM wamnyonge lakini Ruzuku hawatapata mpaka wakaguliwe. Bofya hapa umsikilize
Posted by Bigie habari za kitaifa 12:31 AMSerikali yatangaza kuanza kutumia Ndege za kivita zisizo na marubani ili kutokomeza Majangili
Posted by Bigie habari za kitaifa 12:23 AMTATIZO la ujangili ambalo limekuwa sugu nchini kwa muda mrefu sasa linaanza kupata dawa, baada ya Serikali kutangaza ‘Operesheni Tokomeza’ itakayotumia mbinu za kijeshi.
Katika operesheni hiyo inayotekelezwa kwa awamu, ndege za kivita zisizokuwa na marubani (Drones), zitatumika katika kufanikisha vita hiyo, iliyolenga kunusuru wimbi la wanyama kuuawa.
Akizungumza na RAI katika mahojiano maalumu jana, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, alisema operesheni hiyo itatokomeza ujangili hususan wa tembo ambao umekuwa ukishika kasi kutokana na ukubwa wa soko.
Balozi Kagasheki alisema operesheni hiyo imepata nguvu, baada ya silaha za kupambana na ujangili zilizokuwa zimezuiliwa bandarini kutolewa kwa agizo la Rais Jakaya Kikwete.
Kagasheki aliendelea kueleza mbali ya askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), operesheni hiyo pia itahusisha askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), katika kukabiliana na mtandao huo.
“Ninachotaka kusema katika hii vita, Serikali haitashindwa na kazi ambayo tumekuwa tukiifanya, kila mmoja wetu anajua nini kinachoendelea, nawaomba wananchi waendelee kutupa ushirikiano,” alisema.
Kwa mujibu wa Kagasheki awali oparesheni hiyo ilikuwa ni kukusanya taarifa mbalimbali, ambapo wizara yake imebaini kuwa baadhi ya vigogo wa Serikali wamekuwa wakijihusisha na biashara hiyo.
“Ninawaambia katika hili yeyote atakayekutwa hatasalimika, kwani siwezi kukaa kimya huku wanyama ambao ndiyo urithi wa Taifa wakiendelea kumalizwa na majangili ambao wana nia ovu na Tanzania yetu,” alisema Balozi Kagasheki.
Kuhusu ndege za kivita, Balozi Kagasheki alisema hiyo ni mbinu nyingine katika operesheni hiyo ambapo ndege maalumu ambazo hazina rubani zitakuwa zikizunguka katika maeneo yote ya hifadhi za Taifa na mapori ya akiba.
“Hizi ndege tutazitumia kwa lengo la kuzidisha mapambano na maharamia hawa ambao hivi sasa tunawaambia popote walipo wajue sasa Serikali ipo kazini hasa katika kulinda rasilimali za nchi,” alisema.
Akizungumzia hatua ya Rais Kikwete kuagiza kutolewa kwa silaha zilizokuwa zimekwama bandarini, Balozi Kagasheki alimpongeza rais kwa hatua hiyo ambayo alisema inalenga kujali maslahi ya taifa zaidi.
Hatua hiyo imekuja miezi kadhaa baada ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kudai kodi ya uingizaji wa silaha hizo zilizonunuliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ajili ya kuimarisha vita hiyo.
Kagasheki, alisema hatua ya TRA hapo awali haikuwa sahihi kwani silaha hizo hazikuingizwa kwa ajili ya kumlinda yeye na familia yake, isipokuwa ni kwa ajili ya kulinda rasilimali za nchi.
“Uamuzi wa TRA ulimshangaza Rais Kikwete, baada ya kupata maelezo ya kina kuhusu hali hii alitoa agizo ili sihala hizo zitolewe bandarini mara moja.
“Ni vema jamii ikatambua kuwa tunachofanya ni kuimarisha ulinzi dhidi ya rasilimali za nchi yetu ambayo si mali ya mtu mmoja wala mali ya Kagasheki.
“Katika hili ni lazima kila mmoja atambue kuwa ana jukumu la kutoa taarifa juu ya ujangili huu unaofanywa dhidi ya tembo wetu waliopo katika hifadhi za Taifa pamoja na mapori yote ya akiba.
Waziri Kagasheki pia alilaumu hatua ya Ofisa Upelelezi Mkoa wa Arusha (RCO), Duwan Nyanda, kwa kuruhusu kuachiwa kinyume cha sheria majangili wawili kutoka nchini Saud Arabia.
“RCO huyo wa Arusha akaona haitoshi akaamuru watu hawa ambao walikuwa wamefanya vitendo vya ujangili watolewe na wakabidhiwe na hati zao za kusafiria, kwa hili hapana na wala siwezi kukubaliana nalo hata kidogo.
“Nitafanya mawasiliano na waziri mwenye dhamana ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ili kumweleza kwa kina jambo hili kuhusu kitendo hiki ambacho si cha kuungwa mkono hata kidogo kutokana na vita hii ya ujangili,” alisema.
Kwa mujibu wa takwimu kumekuwa na ongezeko la biashara ya meno ya tembo, ambapo kati ya mwaka 2008 hadi 2009 bei ya Kilo moja ya meno ya tembo ilikuwa ikiuzwa dola 10 na sasa imepanda hadi kufikia Dola za Marekani 1500 hadi 2000.
Kwa mujibu wa Kagasheki, soko kubwa la biashara hiyo hivi sasa lipo katika nchi za China, Vetnam na Thailand.
Aprili 29, mwaka huu katika Mkutano wa Bunge la Bajeti Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli alitaka TRA iachie silaha hizo ili kurahisisha vita dhidi ya ujangili.
“Kamati inaona kwamba japokuwa Wizara ya Maliasili na Utalii, imeonesha nia ya wazi ya kukabiliana na ujangili, na kununua silaha za kufanikisha azma hiyo, Serikali hiyo kupitia TRA imezuia silaha hizo bandarini ikidai kodi,” alisema.
Alisema kuzuiwa kwa silaha hizo za kisasa ni jambo la kushangaza kwani pamoja na wanyamapori ambao ni mali ya Serikali inayoiingizia mapato, bado taasisi kama TRA haioni jitihada za mkono mwingine wa Serikali wa kuokoa rasilimali ya taifa.
Kwa mujibu wa Lembeli tembo wasiopungua 30 huuawa kila siku, huku takwimu za Taasisi ya Utafiti wa Wanyama (TAWIRI ), zikibainisha wazi tishio kubwa na tembo kumalizika.
-Mtanzania
Wanasayansi watabiri kuwa Mwisho wa dunia huenda ukawa tarehe 26/8/ 2032.....Bofya hapa
Posted by Bigie habari za kitaifa 12:16 AMDunia tunayoishi, inaweza kufikia mwisho wake August 26, 2032. Kwa mujibu wa wanajimu wa Ukraine, kimondo chenye upana wa futi 1,300 kinakuja kwa uelekeo wa duniani na kinaweza kuiponda dunia kikiwa na nguvu kubwa ya nuclear.
Crimean Astrophysical Observatory wamegundua kimondo kikubwa kiitwacho 2013 TV135, weekend iliyopita na tayari jumuiya ya kimataifa ya wanasayansi imekielezea kama moja ya vimondo hatari kabisa kuwahi kugunduliwa angani.
Hata hivyo, bado, uwezekano wa kitu hicho kuiponda dunia ni mdogo na hivyo kuna asilimia 99.9984 za maisha kuendelea kama kawaida. Kama kimondo hicho kikiikosa dunia, kina uwezekano wa kupita ndani ya maili milioni 1 za mzingo (orbit) wa sayari hiyo.
Kama 2013 TV135 ikigongana na dunia kinakadiriwa kuzalisha megatons 2,500 za mlipuko.
Hata hivyo kimondo hicho ni kidogo kuliko kitu kilichoiponda dunia na kuwaua wanyama wa zamani aina ya dinosaurs miaka milioni 65 iliyopita. Kimondo hicho kilikuwa na upanda wa maili 6.
Kimondo hicho kitakuwa kimesogea zaidi mwaka 2024, na hivyo kuwaruhusu wanasayansi kuuchambua mzingo wake na wapi kitaangukia. Hadi sasa, kimondo cha 2007 VK184 ndicho kinaaminika kuwa na nafasi ya kuiponda dunia.
Kimondo hicho chenye upana wa futi 420 kitakutana na dunia mwaka 2048.
Source: Daily Mail via bongo5
Mnenguaji wa Mashujaa Band (Nyamwela Jr ) atiwa mbaroni kwa kosa la kumlawiti mtoto wa kiume wa miaka 6
Posted by Bigie habari za kitaifa 8:24 PMMNENGUAJI wa kiume wa Mashujaa Band, Juma Nyamwela (Nyamwela Jr) amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa kiume wa umri wa miaka sita.
Kwa sasa mnenguaji huyo yupo kituo cha polisi cha Mabatini Kijitonyama jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku ya tatu tangu akamatwe kwa tuhuma hizo.
Habari za uhakika kutoka kituoni hapo zinasema katika maelezo ya awali, mnenguaji huyo amekiri kosa.
Chanzo cha salute5 kimeeleza kuwa huenda mnenguaji huyo akafikishwa mahakamani siku ya Jumatatu.
Nyamwela ambaye ni mdogo wake na Super Nyamwela wa Extra Bongo, aliwahi kuitumikia TOT Plus kabla ya kujiunga na Mashujaa Band.
Mwaka 2007 aliibuka bingwa wa mashindano ya dansa bora wa kiume yaliyoandaliwa na Usher Family na kujinyakulia zawadi ya gari.
Source: Salute5.com
CHADEMA yamwaga nyaraka za siri kumjibu Zitto Kabwe...Yawataka Msajili wa vyama na CAG wawajibike
Posted by Bigie habari za kitaifa 11:20 AMHii ni taarifa ya Chadema:
Kutokana na taarifa zilizotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali kuwa vyama vya siasa ambavyo vinapata ruzuku kutoka serikalini havijawasilisha taarifa yake ya mapato na matumizi kwa ajili ya kufanyiwa ukaguzi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa kipindi cha miaka minne mfululizo, yaani kuanzia mwaka 2009/2010- 2012/2013.
CHADEMA tunapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo juu ya taarifa hizo;
i. Kuwa taarifa hizo sio sahihi na hazina ukweli kuhusiana na CHADEMA labda kwa vyama vingine, hii ni kutokana na ukweli kuwa tulishawasilisha taarifa zetu za fedha kwa msajili wa vyama vya siasa na zilizokaguliwa kwa mwaka wa fedha 2010/2011, 2011/2012 na hili linathibitishwa na barua ya msajili wa vyama vya siasa yenye Kumb.Na. CDA.112/123/01a/37, ya tarehe 04 september 2012. Iliyopelekwa kwa makatibu wakuu wa vyama vyote vya siasa (nakala imeambatanishwa).
Aidha, hesabu za mwaka wa fedha zilizokaguliwa za 2009/2010, tuliziwasilisha kwa Msajili wa vyama vya siasa kwa barua yenye Kumb.Na. C/HQ/ADM/MSJ/04/71 ya tarehe 27 Octoba, 2011. (Nakala ya barua imeambatanishwa)
ii. Kuhusu taarifa ya fedha iliyokaguliwa kwa mwaka huu wa fedha 2012/2013, bado haijawasilishwa kwenye ofisi za msajili wa vyama kutokana na barua ya msajili wa vyama vya siasa ya Novemba 26, 2012 yenye Kumb.Na.DA.112/123/16A/97ambayo ilikuwa na maelekezo kuhusu ukaguzi wa mahesabu ya vyama vya siasa, iliyokuwa inajibu barua tuliyomwandikia tukitaka kupata ufafanuzi kuhusu ukaguzi wa hesabu za chama kutakiwa kufanywa na CAG na alitujibu kuwa “tumefanya mawasiliano na Mkaguzi na Mdhibiti wa Mahesabu ya Serikali (CAG) kwa ufafanuzi wa jambo hili na tutawafahamisha ipasavyo kuhusu malipo/gharama mliyotakiwa kulipa katika ukaguzi wa Mahesabu hayo”; mpaka leo hatujawahi kupata ufafanuzi huo pamoja na ukweli kuwa tumeshafunga hesabu zetu za mwaka kama chama (barua imeambatanishwa).
iii. Kuhusu taarifa ya fedha kutoka nje ya nchi, CHADEMA tumekuwa tukiwasilisha taarifa zetu kila mara tunapopata fedha kwa ajili ya mafunzo na programu nyingine mbalimbali za chama kama ambavyo msajili alituandikia barua tarehe 19 Agosti 2013 yenye Kumb. Na.DA.112/123/16a/10 iliyokuwa ni taarifa ya mapato yatokanayo na michango au misaada toka nje ya nchi, alisema “tunashukuru kwa taarifa hii ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa Sheria ya vyama vya siasa” (imeambatanishwa barua husika )
iv.Kuhusu Taarifa za gharama za uchaguzi kwa mwaka 2010 , tuliwasilisha taarifa hiyo na Msajili alikiri kuwa ni vyama viwili tu ndiyo vilikidhi utekelezaji wa sheria ya gharama za uchaguzi kwa ukaguzi wa marejesho, hii inathibitishwa na barua ya Msajili yenye Kumb.Na. CDB.173/205/01/23 ya tarehe 16 April, 2012. (Nakala imeambatanishwa)
Tunapenda kuwahakikishia watanzania kuwa CHADEMA ndiyo ambayo tulidai CAG awe na mamlaka ya kukagua fedha za vyama vya siasa ili taarifa zake ziwekwe hadharani na tutaendelea kutoa ushirikiano kama ambavyo tumekuwa tukifanya siku zote, kuhakikisha sheria hii inatekelezwa ipasavyo kuhakikisha uwazi kwenye mapato na matumizi ya vyama vya siasa.
Aidha, kama ambavyo siku zote tumesimamia na kusisitiza, tunamtaka CAG akague fedha zote za vyama na sio ruzuku tu kama ambavyo kamati ya Bunge inataka iwe.
Imetolewa leo Alhamis, Oktoba 17, 2013;
……………………….
Antony C. Komu
Katibu wa Baraza la Wadhamini.
Jinsi ya kupata Mimba kwa kutumia nguvu za giza (Mitishamba )
Posted by Bigie habari za kitaifa 11:03 AMKabla ya ujio wa wakoloni, babu zetu walikuwa wakiabudu miungu yao.Hakukuwa na dini wala tiba za kisasa.
Kwa kuwa IMANI huponya, ni ukweli usiopingika kwamba maombi yao na tiba zao za asili ziliwasaidia sana katika kutimiza shughuli zao za maisha ya kila siku.
Yafuatayo ni mambo machache ambayo yalikuwa yakipatiwa ufumbuzi kwa nguvu za giza.
1. Kupendwa na mpenzi wako.
-Ili upendwe na mpenzi wako, unachotakiwa kufanya ni kuweka mbegu kavu za nyanya kwenye kitambaa kidogo chekundu au rangi ya damu ya mzee na uwe unaibeba kila siku unapokutana nae au unaweza kuiweka kwenye pochi yake kila unapokwenda kwake.
2:Kujua siri zilizojificha za mpenzi wako.
Kama una mpenzi au mtu ambaye anakuficha jambo na unataka kulijua,chukua viazi tisa,kata katika shepu ya pembe tatu kisha weka chini ya kitanda chako kwa wiki moja, siri zake utazigundua ama kwa kuambiwa na kuoana au yeye mwenyewe atakwambia bila kujijua .
3.Kupata ujauzito.
Ili kupata mbegu zitakazo sababisha mwanamke upate ujauzito,weka vipande vitatu vya mizizi ya mihogo chini ya kitanda kila siku.
Kwa upande wa mwanamke, ili ufanikiwe kumpa ujauzito mwanamke,kunywa juisi ya karoti kila siku huku mawazo yako yote yakifikilia suala hilo.
--Mandai, Uwazi
.
Featured Post
NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne ambayo ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...