Uganda yaongoza orodha ya nchi zinazoridhika zaidi kimapenzi
Posted by Bigie udaku 7:03 PM
Uganda imeongoza orodha ya nchi duniani ambazo wananchi wake wanaridhika zaidi kimapenzi.
Utafiti huo ulifanywa na kampuni inayotengeneza condom, Durex na kuhusisha watu 26,000 kuanzia miaka 16 katika nchi 26.
Katika utafiti huo walibaini kuwa ni watu 44 pekee ndio wanaoridhika
na maisha yao ya mapenzi. Uganda, Switzerland na Hispania ndio
zimeongoza orodha ya watu wanaoridhika zaidi kimapenzi.
Utafiti huo ulibaini kuwa waganda 5 kati ya 10 hushiriki tendo hilo
walau kwa saa moja kila wiki. Hii ilionekana kuwa ni juu zaidi kwa watu
kushiriki tendo hilo duniani.
Tanzania haipo kwenye orodha hiyo.
Hii ni orodha nzima:
1. Uganda
2. Switzerland
3. Hispania
4. Italia
5. Brazil
6. Ugiriki
7. Uholanzi
8. Mexico
9. India
10. Australia
11. Ujerumani
12. China
Wafuasi wa UKAWA Wavamia Msafara wa Magufuli Jijini Arusha Huku Wakiimba Lowassa!!!.....Lowassa!!........Mabomu Yarindima, 6 Watiwa Mbaroni
Posted by Bigie 6:57 AM
Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) yuko jijini Arusha ambapo jioni yupo katikati ya jijini hilo ndani ya uwanja wa Sheikh Amir Abeid, akinadi sera za chama chake.
Kabla ya kufanya mkutano kwenye uwanja wa Sheikh Amir Abeid jioni hii, Dk.
Magufuli alielekea kwanza wilayani Monduli leo asubuhi ambako alitafanya kufanya
mkutano wa hadhara katika eneo la Mto wa Mbu kwa mujibu wa ratiba yake.
Taarifa tulizozipata zinaarifu kuwa hali haikuwa nzuri katika eneo hilo la Mto wa Mbu baada ya msafara wake kukumbana na wafuasi wa UKAWA ambao walivamia msafara huo na kuanza kushangilia wakisema Lowassa!!!....Lowassa!! Lowassa!!! huku wakiwa wamenyoosha vidole viwili juu.-Tazama Video Hii
Mkatafute pa humea hatuitaji pushap tunataka dawa mahospitali maisha bora na elimu bora
Posted by Pearsis Mwetha on Tuesday, October 6, 2015
Hali hiyo iliwafanya polisi waingile kati kwa kupiga mabomu ya machozi ambapo vijana kadhaa wametiwa mbaroni wakituhumiwa kuhujumu mkutano huo wa Magufuli.- Tazama na Hii
Mbali na matukio hayo, Magufuli amefanikiwa kuliteka jiji la Arusha na Watu wamefurika vya kutosha ndani ya uwanja wa Sheikh Amir Abeid
Ccm arusha haina nafasii ni mda huu maandalizi ya magufuli ndo tunampokea namna hiii
Posted by Pearsis Mwetha on Tuesday, October 6, 2015
Breaking News: Mch. Christopher Mtikila afariki kwa ajali ya gari mkoani Pwani
Posted by Bigie habari za kitaifa 12:14 AM
Mwenyekiti wa chama cha siasa (Democratic Party - DP) nchini Tanzania, Mchungaji Christopher Mtikila
amefariki dunia alfajiri ya leo katika ajali ya gari iliyotokea kwenye
kijiji cha Msola mkoani Pwani. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jaffar
Mohamed amethibitisha.
RPC
Mohamed amesema Mtikila alikuwa akitokea Morogoro kuelekea Dar es
Salaam na alikuwa na watu wengine watatu katika gari hilo ambao
wamejeruhiwa.Amesema chanzo cha ajali hiyo bado kinachunguzwa.
Faiza Ally awashukia wanaomkashfu Wema Sepetu na Mhe. Lowassa
Posted by Bigie udaku 10:06 PMMwanamitindo nchini Tanzania, Faiza Allly, ameonesha kuguswa na maneno ya kejeli wanayorushiwa Wema Sepetu na mgombea urais kwa kivuli cha UKAWA, Edward Lowassa na kuwataka watu hao kuuvaa uhusika na kuwa na hofu ya Mungu.
Amesema kuwa hakuna anayeomba ulemavu au kuomba ugonjwa fulani umpate na kudai kuwa baadhi ya watu wanaomsema mgombea urais Lowassa, kupitia ugonjwa wake ni kumkosea haki na sio uungwana.
Sambamba na hilo amesema kuwa mwanadada Wema Sepetu, hatakiwi kulaumiwa kwa kukosa mtoto lakini kubwa ni kumuombea kwani naye anatamani sana kuwa na familia yake, lakini kutokana na matatizo ambayo ni nje ya uwezo wake hadi leo hajapata familia yake.
Amesema kusambaza picha akiwa amebeba mbwa na mwanadada Zari, kuonekana amebeba mtoto ni udhalilishaji kwani kila jambo hupangwa na Mungu hakuna ajuaye kesho yake.
Amedai yeye mwenyewe aliwahi kuzushiwa kuwa na ugojwa wa Ukimwi, na kudai kuwa alijisikia vibaya sana na aliwaza endapo ni kweli angekuwa na ugonjwa huo angekuwa katika hali gani.
Amedai kuwa wanaosema vilema vya wenzao na kuficha vya kwao, wakumbuke kuwa hawawatendei haki watu hao, kwani kwa kuandamwa huko huenda matatizo yakazidi kuongezeka na kufikia hatua mbaya zaidi.
Ameongeza kuwa ni vema wakatumia kitu kingine kuweza kufikisha ujumbe wao na sio kutumia matatizo au magonjwa ya watu kwa maslahi yao binafsi.
Aidha, Mhe. Lowassa amekuwa akikashfiwa sana na baadhi ya watu wa chama tawala kwa madai ya kuwa ni mgonjwa na ugonjwa huo unampelekea kupoteza kumbukumbu na kuishiwa nguvu.
Kwa upande wa mwanadada Wema, amekuwa akishtumiwa kuwa ni mgumba na hivyo kutokana na tatizo hilo ataishia kufuga mbwa wakati wenzake wakiendelea kuongeza familia.
Lowassa: Nataka kura milioni 14
Posted by Bigie habari za kitaifa 9:42 PMMGOMBEA urais aliyeteuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwakilisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Edward Lowassa ametangaza rasmi kuwa ana shida ya kura milioni 14 ili atangazwe rais mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Lowassa alitaka wale wanaomuunga mkono kote anakopita tangu kuanza kampeni kwa ajili ya uchaguzi wa Oktoba 25, wajitokeze kwa wingi na kumthibitishia kumpenda kwa kumpigia kura nyingi.
Alisema iwapo watazipiga kwa wingi siku hiyo, wabaya wanaopanga kumuibia kura zake, hawatafanikiwa kwa sababu watajikuta wakizidiwa na kura alizopigiwa na Watanzania.
“Nipigieni sana kura zenu, nataka kura milioni 14 na ushei ili kuwa rais mpya wa serikali ijayo ya watu itakayoongozwa na watu walio makini,” amesema huku akijinasibu kuwa anagombea urais kwa sababu ana uwezo wa kuwa rais na amechoshwa na umasikini unaowaumiza Watanzania.
“Tutaongoza kwa umakini mkubwa, hatutaki fujo zozote sisi, ni chama cha watu makini. Mimi nagombea urais kwa sababu naweza kuwa rais, nimechoka kuona watu wanalalia mlo mmoja kwa siku, nimechoka, na nina hasira za kupambana na umasikini. Ndio maana nasema kipaumbele change cha kwanza cha pili na cha tatu itakuwa ni elimu ambayo ndiyo inayowatoa wananchi katika umasikini,” amesema mara baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuwataka wananchi wasilale baada ya kupiga kura.
Mbowe alisema safari hii hakuna mtu kwenda kulala akishapiga kura. “Piga kura yako na ukishatoka nje ya kituo, hesabu hatua moja, ya pili na ukifika hatua mia moja hapo kaa ulinde kura.
“Hatutalala na hatutaacha kukesha kulinda kura zetu,” alisema na kupokewa kwa sauti kubwa ya kuungwa mkono na umma uliofika kwenye mkutano huo wa mwisho katika kampeni ya Lowassa mkoani Dar es Salaam.
Mbowe ambaye anatetea kiti cha ubunge jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro, alisema UKAWA hawatakubali ujanja wa Jeshi la Polisi kutaka watu wasikae vituoni wakishapiga kura, kwa sababu hakuna atakayezilinda kura za mgombea wa Ukawa kutokana na mfumo uliopo wa ulinzi.
Wakati huohuo, Waziri Mkuu mstaafu awamu ya tatu, Frederick Sumaye alisema moja ya sababu kubwa zinazomfanya mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli kukosa sifa ya kuchaguliwa, ni kukurupuka katika maamuzi.
Akizungumza katika viwanja vya Tanganyika Packers, jimboni Kawe, Sumaye alisema zipo rekodi nyingi za Magufuli zinazothibitisha kuwa amekuwa mkurupukaji na hivyo kusababisha hasara kubwa kwa taifa.
“Hata mwenyewe amekata tamaa, ameanza kutetea safari za nje za Mheshimiwa Kikwete, hivi rais anawezaje kukaa nje ya nchi kwa zaidi ya nusu ya muda wake aliokaa madarakani? Haiwezekani hizo safari zote zikawa na manufaa kwa Watanzania, kwa kutetea kwake safari hizi, kuna hatari na yeye akafuata mkumbo huohuo,” amesema Sumaye.
“Nchi hii Lowassa akiingia madarakani zaidi ya Sh. bilioni 900 zinatakiwa zilipwe kama faini kwa kuchelewesha kuwalipa wakandarasi, hasara hii imesababishwa na Wizara ya Magufuli na kuna hasara kuhusu meli aliyoikamata ambayo serikali imeshindwa kesi na kudaiwa fidia ya Sh. Bilioni 3.2, amenunua meli mbovu na chakavu akidhani ni mpya, leo hii kwa aibu ile meli haifanyi kazi tena Dar,” amesema.
“Ni mtu huyuhuyu ambaye alitaka kubomoa mpaka jengo la TANESCO wakamuwahi na kumshika shati, yeye hajui kama hilo jengo ni mabilioni ya walipa kodi yametumika kujenga, anajua kubomoa tu matokeo yake mpaka wanamshika shati alishabomoa jengo la serikali la TANROAD na katika kuthibitisha kuwa zilikuwa pupa jengo hilo limeanza kujengwa upya palepale lilipovunjwa,” amesema kabla ya kuongeza:
“Magufuli ni mtu wa maamuzi ya pupa sana. Katika nchi zinazofuata utawala bora alitakiwa kulipa hizo gharama… sasa huyu anataka urais, tumeona akiwa waziri tu anakurupuka na watu wanawahi kumshika shati, hivi akiwa Rais nani atamshika Rais shati?”
Ziara ya kampeni ya Lowassa akifuatana na Sumaye, leo inatarajiwa kuingia mkoani Manyara, nyumbani kwao Sumaye ambaye alikuwa mbunge wa Hanang’ kwa miaka kumi akiwa waziri mkuu.
Lowassa Aweka Wazi Atakakozipata Fedha Za Elimu Bure Hadi Chuo Kikuu.
Posted by Bigie habari za kitaifa, lowassa, siasa 9:34 PM
“Usiniulize hela nitapata wapi? Za kutoa elimu bure Tanzania pesa nyingi
zipo serikalini.
Kama waliopo madarakani sasa wana uwezo wa kuwanunulia
wanawake na ndugu zao nyumba za kuishi kwanini tukose za kutolea elimu
bure?” Lowassa aliyasema hayo katika mkutano uliofanyika katika uwanja wa TP Sinza jana jijini Dar.
MAFURIKO: Picha 40 za Mikutano yote ya Lowassa Leo Jijini Dar es Salaam
Posted by Bigie 8:09 AMNEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini
Posted by Bigie siasa 5:37 AMTume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne ambayo ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja na Mara.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo ofisini kwake Dr. Sisti
Kariah amesema kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha
uandikishaji kwa BVR katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na
Mara zoezi ambalo lilitarajiwa kuanza leo na badala yake zoezi hilo
litafanyika kuanzia tarehe 16/06/2015.
Uamuzi wa kusogeza mbele unafuatia mabadiliko ambayo yanaendelea
kufanywa na Mipaka ya kiutawala ya kata, Vijiji, Vitongoji na Mitaa.
Uandikishaji kwa kutumia mfumo wa BVR unatoa fulsa kwa wananchi wote
wenye sifa za kuwa wapiga kura na wale walio na kadi za Mpiga watatakiwa
kujiandikisha upya.
Zoezi la Uboeshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga
hivisasa limefikia asilimia 50 kwa maana ya mikoa iliyofikiwa na zoezi
hilo nchini Tanzania.
Membe: Nikiwa Rais Wasanii Wataenda Kujifunza Nje
Posted by Bigie siasa 8:43 PM
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe,
amesema kama atachaguliwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, atahakikisha anasimamia haki za wasanii ipasavyo.
Membe alitoa kauli hiyo mkoani Lindi wakati akitangaza nia ya kuwania
urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
“Nitahakikisha naweka mipango imara katika kusimamia kazi za wasanii wote kunufaika na hakimiliki zao,” alisema.
Pia alisema atahakikisha wasanii wanakwenda kujifunza nje ya nchi
masuala ya sanaa ili sekta hiyo ipate mabadiliko ya kimaendeleo kwa
wasanii na Serikali kwa ujumla.
“Nikichaguliwa kuwa rais, nimejiwekea mikakati mingi kuhakikisha sekta
ya sanaa inapiga hatua kutoka hapa tulipo sasa,” alisema Membe.
Katika mkutano huo, waliohudhuria ni baadhi ya wasanii akiwemo
mchekeshaji, Adam Melele ‘Swebe’, Hemed Malyaga ‘Mkwere Orijino’ na
Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Gazeti la Mtanzania
Mama Amchoma Mikono Mwanae kwa Madai ya Kuiba Ugali
Posted by Bigie habari za kitaifa 1:28 PM
Stamili Mponzi mkazi wa kijiji cha Ikule wilayani Kilombero, mkoani
Morogoro anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumchoma mwanae na
kumjeruhi mikono kwa madai ya kuiba ugali.
Mama huyo alimuunguza mwanaye Joseph Chawala, akimtuhumu Kuiba Ugali, kwa mujibu wa watendaji mbalimbali wa kata ya Mng’eta.
Wakizungumzia tukio hilo Jerome Chulu na Jeneth Hetela, walisema unyanyasaji huo ulishuhudiwa na majirani wa mwanamke huyo baada ya kusikia kelele za watoto ambao walimchukua mtoto huyo kumpeleka ofisi ya mtendaji wa kata,polisi na baadaye hospitali.
Walibainisha baadaye kuwa polisi walikwenda kumkamata mwanamke huyo na mumewe Halidi Kiwenji ambaye inadaiwa alikuwa karibu wakati wa tukio hilo ingawa baadaye baba huyo aliachiwa ili akawaangalie watoto wengine nyumbani.
Polisi walithibitisha tukio hilo ambalo uchuguzi wake unaendelea ili kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo.
Wananchi mbalimbali waliohojiwa wametaka hatua kuchukuliwà kwa watu wanaoendekeza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
Mama huyo alimuunguza mwanaye Joseph Chawala, akimtuhumu Kuiba Ugali, kwa mujibu wa watendaji mbalimbali wa kata ya Mng’eta.
Wakizungumzia tukio hilo Jerome Chulu na Jeneth Hetela, walisema unyanyasaji huo ulishuhudiwa na majirani wa mwanamke huyo baada ya kusikia kelele za watoto ambao walimchukua mtoto huyo kumpeleka ofisi ya mtendaji wa kata,polisi na baadaye hospitali.
Walibainisha baadaye kuwa polisi walikwenda kumkamata mwanamke huyo na mumewe Halidi Kiwenji ambaye inadaiwa alikuwa karibu wakati wa tukio hilo ingawa baadaye baba huyo aliachiwa ili akawaangalie watoto wengine nyumbani.
Polisi walithibitisha tukio hilo ambalo uchuguzi wake unaendelea ili kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo.
Wananchi mbalimbali waliohojiwa wametaka hatua kuchukuliwà kwa watu wanaoendekeza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
Dina Marious wa Clouds FM Aamua Kufunguka..Kumbe Amewekwa Benchi Kutangaza..
Posted by Bigie udaku 1:06 PM
Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Mtangazaji Dina Marious Amefunga Mengi
kuhusa hali yake na nini kinaendelea kwenye Ajira yake baada ya muda
mrefu kuwa kimya:
Ameandika Haya:
'Katika haya maisha hamna kitu kibaya kama kumuonea na kumnyanyasa mtu
ambaye hana hatia.Kwa kutumia cheo,madaraka,nguvu na nafasi uliyonayo
ukiamini huyo mtu hana uwezo wa kukufanya lolote
Tunaishi katika dunia ambayo binadamu wamekosa utu na imani.Binadamu
wamekuwa wanyama na makatili kuliko wanyama wenyewe.Unaweza ukakutana na
simba na chui porini mkakaa mkatia story lakini sio binadamu.
Unafanyiwa unyama eti kisa wanataka revenge kwa mtu wako wa karibu.Ambae
revenge hiyo wala haimuathiri lolote zaidi ni kukutesa wewe
kisaikolojia siku hadi siku.
Mbaya zaidi sikustahili miaka yote nimejituma,nimejitoa,sijawahi kumvunjia heshima alokuwa juu yangu kwa ngazi zoote.
Ndugu zangu nimeishi kwa muda mrefu katika huzuni,msongo wa mawazo.Na
hapa niliponimedevelop na vidonda vya tumbo.Nimekuwa na kitu kifuani
kimenikaaa kila siku nahisi nisiposema nitakufa.Ningekuwa nimetendewa
haki isingeniuma wala kunisumbua ni kwa sababu nimeonewa sanaa tena
katika kipindi kibaya sana.
All this time nimekuwa mnyenyekevu na najichekesha nakujitabasamisha
machoni pa watesi wangu.Na wao wakiendelea kunikanyagia chini bila
huruma huku wakinichekea.
Leo nimeamka nina huzuni sana sana na ninahuzunika hasa ninapokutana na msg za kuniuliza niko wapi?mbona sisikiki??
Mimi bado ni muajiriwa na ninalipwa mshahara ila nimewekwa benchi tu.
Kuna kitu naomba nikiweke clear kumekuwa na maneno mengiiiiii
yanazunguka kuwa nina ugomvi na Zamaradi.Mimi sina ugomvi na Zamaradi
sijui ndio amechangia mimi kutolewa kwenye leo tena.Thats not true wala
nguvu hiyo hana.Sijajua why watu husema hivyo ila sina ugomvi nae.Hata
yeye anajua hatuna ugomvi wowote.Nilipotoka pale niliamua kubadili mfumo
wangu wa maisha hivyo hatuna ukaribu kama zamani.Ila haimaainishi tuna
ugomvi.
Na malizia kwa kusema sipo radio wala sipo tv kwa sasa.Maswali
mnaniuliza kila siku na nina wajibu kila mara na leo nimewajibu tena.
ila nitakuwa kwa radio na tv hapo baadae acha niuze mafuta ya
nazi.Maelezo ya mwanzo yamejitosheleza sanaa na sitaenda mbalii sanaa
labda nikiandike kitabu ndio yatatimia.
Nimeandika haya kwa ufupi mjue hata sisi pamoja na majina tuliyonayo
changamoto zipo na tunakabiliana nazo.Na ipo siku tutashinda maana
mtetezi wetu yu hai ' Dina Marious
JK aaga Watanzania ughaibuni
Posted by Bigie siasa 1:46 AM
RAIS Jakaya Kikwete ameendelea kuaga Watanzania kila anapopata fursa
ya kukutana nao, huku mafanikio ya miaka kumi ya uongozi wake
yakijidhihirisha katika maeneo mbalimbali, ikiwemo katika Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambako Bajeti ya Serikali kupitia
wizara mbalimbali imekuwa ikijadiliwa na kupitishwa.
Mwishoni mwa wiki hii akiwa jijini Stockholm nchini Sweden
alikokwenda kwa ziara ya siku tatu, ambayo pia ni ya kwanza ya kuaga
nchi wahisani, Rais Kikwete alikutana na Watanzania waishio nchini humo,
ambako kabla ya kuwaaga, alielezea changamoto anazoziacha.
Rais Kikwete katika mazungumzo hayo, amesema Rais ajaye anakabiliwa
na changamoto ya kuhakikisha Tanzania inayoundwa na Muungano wa nchi
mbili, inaendelea kuwa moja kwa kudumisha umoja wa Watanzania na amani.
“Hapa tulipofikia lazima tuhakikishe Taifa linakuwa moja, kuna vyama
na makabila mbalimbali, lakini lazima tuhakikishe nchi inabaki moja,”
amesisitiza Rais Kikwete.
Rais Kikwete pia alielezea matumaini yake kuwa Tanzania itapata
kiongozi mzuri na kuelezea mafanikio ambayo Serikali yake imeyapata na
kutumaini kuwa yatadumishwa na kuendelezwa na Rais ajaye.
Uchumi Awali akizungumzia mafanikio yaliyopatikana katika uchumi
alipokutana na Waziri Mkuu wa Sweden, Stefan Lofven, Rais Kikwete
alisema uchumi wa Tanzania umekua kwa wastani wa asilimia 7, katika
kipindi cha miaka 10 iliyopita.
Mbali na kukua kwa uchumi wastani, pato la Taifa limekua kwa zaidi ya
mara tatu, kutoka Dola za Kimarekani bilioni 14.4 hadi kufikia Dola
bilioni 49.2 za Marekani.
Aidha, pato la mtu mmoja mmoja kwa mwaka 2005, wakati Rais Kikwete
alipokuwa akiingia madarakani lilikuwa Dola za Marekani 375, lakini
mwaka jana lilifikia Dola za Marekani 1,038.
Mafanikio hayo kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, zilisababisha Waziri
Mkuu wa Sweden, Lofven, kuona umuhimu wa kuanzisha awamu nyingine ya
uhusiano katika maendeleo, utakaoleta maana zaidi.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo Sweden (SIDA),
Torbjorn Pettersson, ambaye pia alikutana na Rais Kikwete, alieleza kuwa
Sweden imeridhishwa na kiwango cha maendeleo na juhudi za kupunguza
umaskini nchini Tanzania.
Hata hivyo, Rais Kikwete alipokuwa akizungumzia kasi ya kuondoa
umasikini, alisema bado juhudi za kuondosha umaskini zinahitajika na
zitafanikiwa kwa kuelekeza nguvu kwenye kilimo, ambacho ndicho
kinachoajiri na kutegemewa na Watanzania wengi zaidi hasa wanaoishi
vijijini.
Rais Kikwete pia amefanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Sweden,
Urban Ahlin, pamoja na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa nchini
humo na kushukuru kwa misaada ya maendeleo kwa takribani miaka 50 sasa.
Viongozi hao wamempongeza Rais kwa kufanya ziara ya shukrani na
kuwaaga, kwani ni mara chache kwa viongozi wengi wa Kiafrika kuaga na
kuondoka madarakani.
Mbali mazungumzo hayo ya Sweden, mafanikio mengine ya Serikali kwa
miaka 10 iliyopita, kwa wiki ya tatu sasa yamegeuka nguzo mbuhimu ya
kutetea bajeti za wizara mbalimbali bungeni na katika warsha mbalimbali.
Afya Kwa mfano katika wiki hii katika sekta ya afya, Waziri wa Afya
na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid alipokuwa akizungumza na wahariri wa
vyombo vya habari, aliwataka kusoma takwimu za mafanikio ya Tanzania
ikilinganishwa na nchi zingine badala ya kuishia kusoma bajeti ya sekta
hiyo pekee.
Kwa mujibu wa Dk Rashid, pamoja na Tanzania kuwekeza asilimia 2.8 tu
ya pato la Taifa katika sekta ya afya, vifo vya watoto chini ya miaka
mitano vimepungua na mafanikio hayo ni makubwa kuliko katika nchi
zinazoonekana kupiga hatua zaidi katika uwekezaji huo.
Alitaja nchi ya Botswana yenye uwekezaji wa asilimia 3 ya pato la
Taifa katika afya na Zambia yenye asilimia 4.2 ya pato la Taifa katika
sekta hiyo, kwamba mataifa hayo katika kila vizazi hai 1,000 wamekuwa
wakipoteza watoto wengi zaidi.
Wakati Tanzania ikipoteza watoto 52 katika kila watoto hai 1,000
wanaozaliwa, Kenya wao wanapoteza watoto 71, Zambia watoto 87 na
Cameroon ni watoto 95 katika kila vizazi haivyo 1,000.
Umeme Katika upatikanaji wa huduma za nishati na umeme, mpaka mwaka
jana, Serikali ilikuwa imefikisha umeme kwa zaidi ya asilimia 35 ya
Watanzania, kutoka asilimia wastani wa chini ya asilimia 15 iliyokuwepo
mwaka 2005.
Akizungumza bungeni jana, Waziri wa Nishati na Madini, George
Simbachawene alisema idadi ya wateja waliounganishiwa umeme vijijini
imefikia asilimia 68. Idadi hiyo imeongezeka kutoka 143,113 mwaka 2013
hadi kufikia wateja 241,401 Aprili mwaka huu.
Alisema wateja hao wameunganishiwa umeme kupitia miradi ya Wakala wa
Umeme Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).
Bomba la gesi Akizungumzia jitihada za kuanza kutumia hazina ya gesi
asilia kwa ajili ya kuzalisha umeme badala ya mafuta mazito
yanayosababisha umeme uwe bei ghali nchini, Simbachawene alisema mitambo
ya kusafisha gesi asilia na bomba la gesi asilia, vitaanza kazi rasmi
Septemba mwaka huu.
Alisema ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka Mtwara kupitia Lindi
hadi Dar es Salaam umekamilika, ujenzi wa mitambo ya kusafirisha gesi
asilia katika eneo la Madimba, Mtwara umefikia asilimia 99 na mitambo ya
Songo Songo, Lindi nao umefikia asilimia 99. “Mitambo na bomba hilo
vitaanza kufanya kazi (Commercial Operational Date) Septemba 2015.
“Haya ni matokeo ya utekelezaji wa miongoni mwa miradi iliyoanishwa
kwenye Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 - 2015/16),” alisema
Simbachawene.
Alisema matumizi ya gesi asilia yatachochea ukuaji wa viwanda,
utunzaji wa mazingira kwa kupunguza matumizi ya kuni na mkaa, kuongeza
ajira na hatimaye kuleta maendeleo ya uchumi na kijamii kwa ujumla.
Elimu Katika elimu, mwaka 2005 wakati Rais Kikwete akiingia
madarakani, Bajeti ya Serikali katika sekta hiyo ilikuwa Sh bilioni 600,
lakini mwaka jana ilifikia Sh trilioni 3.4.
Sababu ya uwekezaji huo mkubwa, Rais Kikwete aliwahi kusema
alipoingia madarakani, alikuta Tanzania yenye watu wengi zaidi katika
nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, iko nyuma ikilinganishwa
na Kenya na Uganda, kwa idadi ya wanafunzi waliokuwa wakisoma shule za
sekondari na vyuo.
Kwa mujibu wa Rais Kikwete, mwaka 2005 wanafunzi waliokuwa wakisoma
sekondari ni zaidi ya 500,000, wakati nchini Uganda waliokuwa wakisoma
sekondari walikuwa zaidi ya 700,000 na Kenya zaidi ya 900,000.
Kwa upande wa vyuo vikuu, Tanzania ilikuwa na wanafunzi 40,000 tu wakati Uganda ilikuwa na wanafunzi 124,000 na Kenya 180,000.
Hatua zilizochukuliwa, Rais Kikwete alisema Serikali kwa kushirikiana
na wananchi, waliamua kujenga shule za sekondari za kata, ambapo
wananchi walihamasishwa, wakahamasika wakajenga shule mpaka Mkurugenzi
mmoja wa elimu, akahofia kukosa walimu wa kupeleka katika shule hizo.
Kwa sasa Tanzania ina wanafunzi 1,800,000 wanaosoma sekondari na
imeshaipita Uganda yenye wanafunzi 1,700,000 wanaosoma elimu ya
sekondari, lakini imezidiwa na Kenya ambayo ina wanafunzi 2,100,000.
Hata hivyo alisema ni rahisi kuipita Kenya kwa hilo pengo la
wanafunzi 300,000, kwa kuwa shule za sekondari zilizopo zina nafasi ya
kuongeza wanafunzi milioni mbili zaidi.
Kwa upande wa elimu ya juu, Rais Kikwete alisema vyuo vikuu
vimeongezeka kutoka 26 mwaka 2005 hadi kufikia 52 na idadi ya wanafunzi
walio katika vyuo vikuu ilitoka 40,719 hadi kufikia 200,956.
Hata bajeti ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu imeongezeka kutoka Sh bilioni 56.1 hadi Sh bilioni 345 mwaka 2014.
Photos: Who Rocked It Better - Agnes Masogange or Linah Sanga?
Posted by Bigie gossip 6:47 AMBUBU Afanyiwa Unyama wa Kutisha......Wanaume Watano Wamteka na Kumbaka kwa Zamu
Posted by Bigie news 6:45 PMMKAZI wa kitongoji cha Chingale, kijiji cha Mtakuja kata ya Temeke katika Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara ambaye ni bubu, Asumini Fakihi amebakwa na watu watano wasiojulikana na kumsababishia majeraha na kulazwa katika Hospitali ya Mkomaindo mjini Masasi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara, Agustino Ollomi alisema juzi saa 1:00 usiku wa mkesha wa Krismasi katika kitongoji cha Chingale, mama huyo alivamiwa na watu hao wasiofahamika waliofanikiwa kumfanyia kitendo hicho na kutokomea kusikojulikana.
Mwanamke huyo hakuweza kuwatambua watu hao mara moja na kwamba baada ya tukio hilo Mwenyekiti wa kitongoji hicho, kwa ushirikiano na wasamaria walitoa taarifa kituo cha polisi Masasi kwa msaada zaidi.
Ollomi alisema polisi walifanikiwa kufika katika eneo la tukio usiku huo wa mkesha wa Krismasi na kukuta mama huyo (39) akiwa hajitambui huku sehemu zake za siri zikiwa na majeraha makubwa na kukimbizwa katika hospitali ya Mkomaindo ambako hadi sasa amelazwa akipatiwa matibabu.
Alisema jeshi la polisi mkoani Mtwara linaendelea kuwasaka watuhumiwa hao na watakapopatikana watafikishwa mahakamani kujibu shitaka hilo linalowakabili.
Hausiboi Aliyelawiti Mtoto wa Miaka 6 Ahukumiwa Kifungo cha Maisha Jela
Posted by Bigie news 6:30 PMMfanyakazi wa nyumbani, Hatibu Adamu (20) amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa kike wa miaka sita.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Said Mkasiwa alisema kuwa upande wa mashitaka ulikuwa na mashahidi watano na kwamba mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa.
Awali, Wakili wa Serikali, Silvia Mitanto alidai mahakamani hapo kwamba kutokana na kuongezeka kwa matukio ya ubakaji nchini, mshitakiwa huyo apewe adhabu kali iwe fundisho kwa wengine.
Kabla ya hukumu hiyo, Adamu alidai kwamba anasumbuliwa na vidonda vya tumbo hivyo aliomba apunguziwe adhabu. Hata hivyo mahakama hiyo haikusikiliza maombi hayo.
Mshitakiwa huyo ambaye ni mkazi wa Majohe, Dar es Salaam, alidaiwa kwamba tarehe isiyofahamika Septemba, mwaka jana, maeneo ya Majohe Wilaya ya Ilala, Adamu alimlawiti mtoto huyo mwenye miaka sita huku akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Matokeo Mabaya ya CCM Singida: Nyalandu Abebeshwa Zigo la Lawama
Posted by Bigie news, politics 6:24 PMBARAZA a Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Singida Vijijini, limemshutumu mbunge wao, Lazaro Nyalandu kwa kusababisha chama hicho kukosa ushindi mnono kwenye baadhi ya maeneo katika jimbo la Singida Kaskazini wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa hivi karibuni.
Katika Kikao cha Baraza hilo kilichoketi mjini hapa juzi kutathmini Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, wajumbe hao walisema kuwa sababu kuu ya baadhi ya maeneo kuchukuliwa na upinzani ni mbunge huyo, ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, kushindwa kutimiza ahadi zake kwa wakati.
Walisema kuwa kati ya vijiji 84 vilivyopo kwenye jimbo hilo, vijiji vinane vimechukuliwa na upinzani wakati kati ya vitongoji 436, vitongoji 49 vimechukuliwa na upinzani.
“Hii ni kutokana na mbunge wetu kuwa na ahadi hewa na kukataa baadhi ya ahadi alizowahi kutoa mwenyewe,” walisema wajumbe.
Akisoma maazimio ya kikao hicho, Mwenyekiti wa UVCCM Singida Vijijini, Shaban Mang’ola alisema kuwa kutokana na hali hiyo wamempa mbunge huyo muda wa siku 14 tu kuweza kufika Singida mara moja kuonana na jumuiya hiyo na kutoa maelezo ya kuridhisha juu ya mustakabali wa ahadi zake.
Aidha, maazimio hayo yanasema kuwa iwapo mbunge huyo atashindwa kufanya hivyo katika muda uliopangwa, UVCCM itaitisha mkutano mkuu wa vijana wa jimbo na kutoa maamuzi watakayaona yanafaa.
Waziri Nyalandu anadaiwa kuhamasisha na kuahidi kuwapatia mikopo vijana zaidi ya 9,000 wa jimbo hilo, ahadi ambayo hajatimiza hadi hivi sasa. Wajumbe walidai kuwa kila kijana aliyetaka kuchukua mkopo aliingia gharama ya Sh 8,000. Pia anadaiwa kuitisha ligi ya mpira wa miguu na kuahidi kuwapatia zawadi washindi lakini baadaye akaikana ligi hiyo.
Aidha, mbunge huyo anadaiwa kuwatukana hadharani baadhi ya wapiga kura wake jambo, ambalo baraza hilo limekiita kuwa ni dharau kwa jumuiya ya umoja huo.
Hata hivyo, Nyalandu akizungumza kwa simu na gazeti hili alisema taarifa hizo hazina ukweli wowote na kwamba kuna watu walilipwa fedha kwa ajili ya kumchafua na kukichafua chama.
“Habari hizi ni za kuchafua tu na uongo. Kuna watu walilipwa na Mwenyekiti huyo wa UVCCM anajua, kisha wakaitisha mkutano kinyume na utaratibu pamoja na waandishi wa habari, wakachaguliwa vijana watano ili kusema hayo waliyosemwa. Kwenye Jimbo langu, CCM imefanya vizuri sana na huo ndio ukweli,” alisema.
Nyalandu ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii alisema katika jimbo lake hilo la Singida Kaskazini, CCM imeshinda vijiji 179 na kushindwa katika vijiji vinane na kuongeza kuwa huo ndio ukweli halisi na kuhoji kuwa kwa idadi hiyo ya ushindi kweli CCM imeshindwa?
Kwa mujibu wa Nyalandu, leo Kamati ya Siasa ya Wilaya inakutana katika mkutano wa dharura ambapo watajadiliana kuhusu mwenyekiti huyo anayedaiwa kuhongwa fedha na kufanya mkutano huo wa vijana usiokuwa rasmi na kwamba moja ya hatua zinazotarajiwa kuchukuliwa dhidi ya Mang’ola ni kusimamishwa na chama.
“Ni watu wenye nia mbaya tu wameamua kuitisha mkutano kinyume cha Sheria. Lakini Kamati ya siasa ya wilaya inaitisha mkutano wa dharura na kuna tamko litatolewa kuhusiana na mwenyekiti huyo, kwa sababu inajulikana kabisa kwamba walipewa hongo kutoa taarifa hizo za uongo,”
BAKWATA Yasisitiza kuwa Maamuzi ya Rais Kikwete kuhusu Sakata la Escrow Yaheshimiwe
Posted by Bigie news 6:15 PMBARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limewataka Watanzania kuheshimu uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete na mamlaka zinazohusika kuhusu suala la akaunti ya Tegeta Escrow.
Kauli hiyo imetolewa na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum ambapo alisema, ni muhimu kwa Watanzania kumuamini Rais Kikwete na kuziachia mamlaka husika kufanya kazi zilizoagizwa.
Akigusia hotuba hiyo, alisema ni hotuba nzuri ambayo imekusanya historia nzima ya fedha za Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na kufafanua kama ni za umma au si za umma, pia imeonesha ukomavu.
Alisema kama Bakwata wanapongeza hotuba ya Rais Kikwete kwani ameonesha ni kiongozi anayetumia hekima na weledi katika uongozi na kutatua matatizo mbalimbali, licha ya kuwepo kwa mashinikizo kutoka kwa watu mbalimbali.
“Kiongozi yeyote hapaswi kukurupuka katika kutoa maamuzi na hilo ndilo alilolionesha Rais Kikwete katika hotuba yake.
“Hakuna sababu ya watu kuandaa maandamano kwani aliyoyasema Rais Kikwete yameeleweka na alieleza kwa upana zaidi, hivyo watu wasitake kumsambazia ubaya hata kwa mazuri anayoyafanya tayari; mamlaka zinazohusika zimepewa majukumu na wengine wamewajibishwa,” alisema Salum.
Alisema pia baraza hilo litaendelea kupinga mambo ambayo yanaonekana kutaka kuchangia kupoteza amani ya nchi, kwa lengo la kuidumisha na kuienzi siku zote.
Watu Wawili Watiwa Mbaroni kwa kukutwa na Meno ya Tembo
Posted by Bigie news 6:07 PMWATU wawili wametiwa mbaroni na Polisi mjini Mpanda kwa kukutwa na meno ya tembo waliokamatwa yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 157 ndani ya basi la Adventure.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alisema vipande
vilivyokamatwa ni 22 vyenye uzito wa kilo 46.3 sawa na tembo saba
waliouawa.
Aliwataja
watuhumiwa hao kuwa ni Justine Baruti (39) mkazi wa kijiji cha Ivungwe –
Katumba katika Kambi ya Wakimbizi kutoka nchi jirani ya Burundi iliyoko
wilayani Mlele mkoani Katavi.
Mtuhumiwa
mwingine ni Boniface Hoza (40) mkazi wa kijiji cha Kalela wilayani
Kasulu mkoani Kigoma. Akisimulia mkasa huo Kidavashari alisema Desemba
24 mwaka huu saa 12:00 alfajiri, askari polisi wakiwa doria katika Kituo
Kikuu cha mabasi kilichopo eneo la Mji wa Zamani mjini Mpanda
walimtilia shaka mmoja wa watuhumiwa Jusitine Baruti ambaye akiwa na
kifurushi tayari kupanda basi la abiria la Kampuni la Adventure.
Inadaiwa
kuwa basi hilo la Adventure lenye nambari za usajili T992 DDT lilikuwa
limepaki katika Kituo Kikuu cha mabasi mjini Mpanda tayari kwa safari ya
kuelekea mjini Kigoma.
“Mtuhumiwa
huyu alijaribu kuwatoroka askari hao wa doria lakini walifanikiwa
kumkamata na kumweka chini ya ulinzi. Walipopekua mabegi mawili
aliyokuwa nayo walikuta vipande 15 vya meno ya tembo vyenye uzito wa
kilo 33. Vipande hivi kwa pamoja vikiwa na thamani ya Sh 90,000,000 ni
sawa na tembo wanne waliouawa,” alieleza.
Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari, basi hilo la abiria liliamriwa kwenda Kituo Kikuu cha Polisi kilichopo mjini Mpanda ambapo baada ya upekuzi wa kina, mtuhumiwa mwingine Boniface Hoza alikamatwa akiwa ameficha begi kwenye uvungu wa kiti alichokalia chenye namba K3.
.
Featured Post
NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne ambayo ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...





















