AGNESS GERALD "MASOGANGE" ACHUMBIWA
agness masogange, BONGO MOVIE, habari za kitaifa, JAMII, picha za utupu 4:47 AM
MREMBO anayeuza nyago katika video za wanamuziki wa Bongo Fleva na muvi za Kibongo, Agness Gerald ‘Masogange’, amechumbiwa nje ya Tanzania.
Akizungumza na mpekuzi wetu juzikati, Agness aliweka kweupe kuwa, amevishwa pete ya uchumba na mwanaume anayemtosheleza kwa kila kitu ambaye siyo Mbongo na kifuatacho ni ndoa itakayofungwa muda si mrefu.
Alifunguka: “Ndoa itafungwa nchini kwa huyo mwanaume, lakini taratibu nyingine zote kama send-off zitafanyika hapa Bongo.”
Agness aliweka wazi kuwa hakuwa tayari kuolewa Bongo kwa sababu wanaume wengi ni wazinguaji na hawana mapenzi ya dhati.
Mrembo huyo mwenye umbo tata alisema kuwa pamoja na kuwaambia amechumbiwa, wanaume wameendelea kumtokea kila kukicha.






