"SINA MPANGO WA KUOLEWA KWA SABABU SITAKI KUWA MFUNGWA NA NINAHITAJI UHURU ZAIDI"......AGNESS MASOGANGE

Picha  ya Agness  alipo achia video yake chafu

WAKATI baadhi ya mastaa bongo wakikataa kuolewa kwa sababu zao binafsi, mrembo anayetamba kwenye video za bongo Agnes Gerald maarufu  kama Agnes Masogange, amedai kuwa kuishi bila mume kunamfanya aishi maisha ya raha, kwani anaamini akiolewa atakuwa kama mfungwa anayesubiri hukumu ya kifo.

Mwanadada huyo ambaye amekuwa akikumbwa na skendo kibao katika maisha yake, amedai kuwa maisha yake yanaenda poa bila hata ya kuwa na mume kwani ishu zake anazofanya zinamfanya aishi maisha mazuri.


“Kuhusu ndoa; Hapana kwa kweli maana ndoa ni kitu cha mwisho sana katika maisha yangu kwani sasa nahitaji kufanya ishu zangu za mjini, ambazo zinanipa maisha mazuri ambayo yananifanya nitoke kwenye umaskini,”
alidai.

Hata hivyo alishindwa kueleza ni kazi gani anayofanya mjini ukiachilia mbali kuwapa tafu wasanii wa bongo kwenye video zao, ingawa alidai zipo ishu kibao ambazo amekuwa anazikifanya za ndani na nje ya nchi.

Posted by Bigie on 6:45 PM. Filed under , , , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.